NJIA YA ASILI YA KUPUNGUZA MAUMIVU YA TUMBO LA HEDHI
JINSI YA KUPUNGUZA MAUMIVU Maumivu ya hedhi hutokea pale tumbo nlinapojikunyata (contract) na kuachia ili kuondoa uchafu uliopo kwenye kuta za endometria. Maumivu ya hedhi hutofautiana kwa baadhi ya wanawake ambapo wengine hupata maumivu makali sana na wengine maumivu ya kawaida. Maumivu ya hedhi yanaweza kuwa makali sana na hata kuathiri ufanyaji kazi wa shughuli mbalimbali kwa siku kadhaa. Wanawake wengi hutumia dawa za maumivu kama panadol kupunguza maumivu yasiyo makali sana na dawa kama naproxen, diclofenac na ibuprofen kupunguza maumivu makali lakini wanatakiwa kufahamu kuwa dawa hizi huweza kusababisha vidonda vya tumbo kwani hukwangua kuta za tumbo hivyo hazipaswi kutumiwa mara kwa mara. Njia za asili unazoweza kutumia ili kupunguza maumivu yanayotokana na mzunguko wa hedhi ni pamoja na; Kupata usingizi wa kutosha na kupumzika, pia kufanya mazoezi mara kwa mara, yoga pamoja na kufanya shughuli ndogondogo husaidia kupunguza maumivu kwa baadhi ya wanawake. Kutumia maji ya moto