NJIA YA ASILI YA KUPUNGUZA MAUMIVU YA TUMBO LA HEDHI

JINSI YA KUPUNGUZA MAUMIVU 

 Maumivu ya hedhi hutokea pale tumbo nlinapojikunyata (contract) na kuachia ili kuondoa uchafu uliopo kwenye kuta za endometria. Maumivu ya hedhi hutofautiana kwa baadhi ya wanawake ambapo wengine hupata maumivu makali sana na wengine maumivu ya kawaida.

Maumivu ya hedhi yanaweza kuwa makali sana na hata kuathiri ufanyaji kazi wa shughuli mbalimbali kwa siku kadhaa.

Wanawake wengi hutumia dawa za maumivu kama panadol kupunguza maumivu yasiyo makali sana na dawa kama naproxen, diclofenac na ibuprofen kupunguza maumivu makali lakini wanatakiwa kufahamu kuwa dawa hizi huweza kusababisha vidonda vya tumbo kwani hukwangua kuta za tumbo hivyo hazipaswi kutumiwa mara kwa mara.

Njia za asili unazoweza kutumia ili kupunguza maumivu yanayotokana na mzunguko wa hedhi ni pamoja na;

Kupata usingizi wa kutosha na kupumzika, pia kufanya mazoezi mara kwa mara, yoga pamoja na kufanya shughuli ndogondogo husaidia kupunguza maumivu kwa baadhi ya wanawake.

Kutumia maji ya moto/uvuguvugu kwa kulowanisha kitambaa safi kwenye maji ya moto na kisha kukanda kwenye sehemu ya chini ya tumbo au kwa kuviringisha chupa yenye maji ya moto tumboni.

Pia kuna baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba utumiaji wa vitamin E, vitamin B-1, vitamin B-6, magnesium au mafuta ya omega-3 unaweza kupunguza maumivu yatokanayo na hedhi hivyo kutumia vyakula kama wali, mkate, maziwa, maparachichi, karanga, njugu za lozi (almond),mayai, mboga za majani kama spinach na broccoli na vyakula vingine vilivyo na vitamin zilizotajwa hapo juu husaidia kupunguza uwezo wa kupata maumivu wakati wa hedhi.

Kupunguza mawazo hasa mawazo yanayotakana na hisia mbalimbali (emotional stress) au mawazo ya kisaikolojia inaweza kupunguza uwezo wa kupata maumivu wakati wa hedhi au kupunguza ukali wa maumivu yanayotakana na hedhi.

Kunywa maji mengi pia husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini hivyo kupumzisha misuli iliyokakamaa au kula vyakula ambavyo vina majimaji kama saladi, matikiti maji na matango hupunguza kwa kiasi kikubwa maumivu ya hedhi

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU