ZIJUE FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA MWILINI

HABARI ZA MUDA HUU WAPENDWA WA MAKALA ZETU, LEO TUNAONGELEA KUHUSU FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA MWILINI .KARIBU NA ENDELEA KUFUATILIA MAKALA ZATU.

HIZI NI FAIDA KUU NNE ZA MBEGU ZA MABOGA MWILINI

   1.  HUONGEZA NGUVU ZA KIUME

Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.
Inatokeaje mbegu za maboga kuongeza nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili.
Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako pia zinaongeza uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona mabadiliko makubwa sana.
         2. ZINAONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama. Mama mjamzito hasa  unayenyonyeshaunashauriwa kutumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.
Pia unaweza kuchanganya unga wa  mbegu za maboga  na uji kwa ajili ya kumpatia mtoto.
          3. NI DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME
Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.
Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama ‘benign prostatic hyperplasia’.
Wanaume kazi ni kwenu.
       4.  ZINAONDOA  MSONGO WA MAWAZO (STRESS)
Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya msongo wa mawazo kiafya.
Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.
Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance).
Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’.
Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.
Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

JINSI YA KUTUMIA
-Unaweza kuzitumia zikiwa zimekaangwa au mbichi. chukua mbegu zioshe tia chumvi kidogo kisha weka jikon kwa mda wa dakika tano ukiwa unazikorogo ili zisiungue kisha epua tayari kwa kulia. pia njia nyingine ni kama ukitaka kutumia zikiwa mbichi,osha mbegu zako vizuri kisha zianike juani kwa mda wa masaa kadhaa zikauke na baada ya hapo unaweza kuzitumia. 


Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU