SABABU ZA MAUMIVU YA KIUNO NA MGONGO


Maumivu haya huweza kusababishwa na matatizo kwenye via vya uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo mkubwa au misuli ya nyonga. Yanaweza kuwa yanaendana na mzunguko wa hedhi au la, huwa mara nyingi chini ya kitovu na kiunoni. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kuathiri shughuli zako za kawaida.

Sababu Za Maumivu ya Kiuno 
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ya kiuno kwa muda mrefu, sababu hizi ni:

Maumbukizi ya ndani ya kiuno ya muda mrefu (Chronic Pelvic Infection).Maambukizi haya hutokana ugonjwa wa TB na huweza kusababisha maumivu ya kiuno.Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ukuta wa uzazi huota sehemu nyingine za uzazi. Huleta maumivu wakati wa hedhi au kufanya mapenzi.Maambukizi ya muda mrefu ya shingo ya uzazi au mji wa uzazi (Chronic endometritis or cervicitis). Husababisha maumivu ya kiuno wakti wowote na wakti wa kufanya ngono.Mimba Kutunga Nje ya Mfuko wa Uzazi (Ectopic Pregnancy)Vivimbe vya kizazi (uterine fibroids).Husababisha maumivu pale ambapo vinakua kwa haraka, vinajiviringisha au kukandamiza ogani nyingine. Maumivu yake huwa ya kuja na kuacha.Maambukizi ya njia ya mkojo ya muda mrefu (Chronic Urinary Tract Infection). Husababisha maumivu hasa wakati wa kukojoa.Maambikizi ya via vya uzazi (Pelvic inflammatory Disease – PID).Maambukizi ya Kibofu cha Mkojo (Interstitial cystitis)Hali hii huleta maumivu hasa chini ya kibofu cha mkojo ambayo hupungua pale unapokojoa.
 Dalili nyingine ni kukojoa mara kwa mara, kukojoa usiku na kushindwa kubana mkojo.Ugonjwa wa Kidole Tumbo (Chronic Appendicitis). Tatizo la kidole tumbo huleta maumivu upande wa kulia chini ya kitovu ambayo huwa hayatulii na dawa za maumivu.Kushikana Kwa Via Vya Uzazi (Pelvic Adhesions)Saratani ya Utumbo Mpana. Tatizo hili huweza kuleta maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu na kiunoni kwa muda mrefu.Ajali Maeneo Ya kiunoni .Ajali huweza kuathiri mifupa.

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU