ZIJUE FAIDA ZA LIMAO MWILINI



Hizi ni faida saba za maji la limau kwa mwili wako.
1. Husaidia kuongeza maji mwilini
Kulingana na wataalamu wa lishe mtu mwenye afya bora anahitaji kunywa maji kati ya lita 2 na 5 kila siku. Maji haya ni pamoja na maji kutoka kwenye vyakula na vinywaji.
Maji ndicho kinywaji bora zaidi cha kuhakikisha mwili una maji ya kutosha, lakini badhi ya watu hawapendi maji kawaida. Kuongeza limau husaidia katika kuyafanya maji kuonya vizuri, na huweza kukupa hamu ya kunywa maji mengi zaidi.
2. Ni nzuri kwa vitamini C
Ingawa sio moja ya matunda yenye virutubisho vingi vya vitamini C, limao ni bora kwa kuwa kemikali mimea ambayo hupatikana katika tunda hilo husaidia kutibu mafua na mfumo wa upumuaji.
Maji ya limao yanatajwa kuwa na takriban miligramu 18.6 za vitamini C. Na vipimo kamili vya kila siku vinavyopendekezwa kwa watu wazima ni kati ya miligramu 65 na 90.
3. Husaidia katika kupunguza uzito wa mwili
Utafiti umeonyesha kuwa virutubisho vilivyo katika limau kwa kiasi kikubwa husadia katika uzito wa mwili na hii ni kutokana na utafiti uliofanywa kwa kutumia panya.
Ingawa haukufanyiwa kwa binadamu ni wazi afiti nyingi zilizofanikiwa ulimwenguni ili kumfaidi binadamu panya ametumika kwa hivyo huenda kuna ukweli..
4 Husaidia kuboresha afya ya ngozi
Vitamini C ambayo hupatikana katika limao husaidia kuboresha afya ya ngozi, fizi (kuzuia fizi kutoka damu, ukavu wa ngozi ikiwemo kupasuka midomo na pua kavu). Pia husaidia kukata uchovu wa mazoezi au marathon.
5. Husaidia katika mmeng'enyo wa chakula
Maji ya limao husaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, kwa hivyo uashauriwa kunywa sharubati yenye mchanganyiko wa limao au ndimu, au bilauri ya maji ya limao au ndimu nusu saa kabla ya kula.
Kwa jumla, maji ya limao ya kutosha mwilini husaidia katika kuhakikisha moyo, figo, misuli, maini na ubongo kufanya kazi inavyostahili kwa kupambana na sumu mbalimbali mwilini.H

6.usaidia kuondoa harufu mbaya
Ngozi ya limao ikitumiwa katika kunawa mikono baada ya kula samaki husaidia kuondoa harufu ya kukera ambayo hubakia kwenye mikono baada ya kula na hata mdomoni baada ya kula vyakula vyenye harufu kali ya vitunguu. Pia glasi moja ya limao kila asubuhi na baada ya chakula itasaidia sana katika kuzalisha mate na hatimaye kuondoa harufu mbaya mdomoni inayoletwa na bakteria.
7. Husaidia kuzuia au kupambana na vijiwe vya figo
Ili kupambana na vijiwe vya figo, gout (mrundikano wa uric acid kwenye viungo na mwili) unashauriwa kunywa maji ya limao ambayo yana tindikali.
Tindikali hiyo husaidia kufyonza na kubadilisha madini ya chuma (ferrous iron) kwenye vyakula jamii ya mimea na kufanya viweze kutumika kutengeneza damu.

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU