JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA MAJI



Vipimo:
Unga wa ngano 2 vikombe (nusu kg)
Mayai 2
Chumvi Kiasi
Kitunguu maji cha kiasi 1
Karoti ya kusaga ( ukihitaji)
Mafuta  ya kupkia Nusu kibakuli
Maji kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Tia maji na mayai kwanza katika mashine ya kusagia (blender) kisha
2. Tia unga, chumvi usage ili unga uchanganyike.
3. Mimina katika bakuli, ikiwa unga mzito, ongeza maji kama uwe mwepesi kiasi.
4. Katakata kitunguu maji na karoti uliyosaga vichanganye
5. Weka kikaango kisichoganda (non-stick frying pan) katika moto na uteke unga kwa upawa wa duara uutandaze vizuri katika kikaango.
6. Subiri Chapati ikauke, igeuze upande wa pili huku unaungandamiza na kuizungusha Chapati katika kikaango ili iive.
7. Iinue kidogo Itie kijiko kimoja cha supu, mafuta au samli.
8. Kakaanga hadi Chapati iive iwe rangi ya hudhurungia kama katika picha.
9. Geuza tena Chapati na igandamize gandamize tena kama dakika moja Iive vizuri upande wa pili bila ya kutia tena mafuta kisha epua uweke katika sahani kuendelea na nyingine

Asanten na karibuni kwenye page yetu kwa mapishi zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU