SABABU, DALILI NA TIBA YA UVIMBE KWENYE KIZAZI

Sababu 1. Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini. 2. Ujauzito. 3. Uzito na unene kupita kiasi. 4. Jenetiki zisizo za kawaida. 5. Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu. 6. Sababu za kurithi. 7. Lishe isiyo sawa. 8. Sumu na taka mbalimbali n.k. dalili 1. Kupata damu nyingi wakati wa hedhi. 2. Maumivu makala wakati wa siku za hedhi. 3. Kuvimba miguu. 4. Unaweza kuhisi una ujauzito. 5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa. 6. Kuhisi kuvimbiwa. 7. Kupata haja ndogo kwa taabu. 8. Kutokwa na uchafu ukeni. 9. Kupata choo kigumu au kufunga choo. 10. Maumivu nyuma ya mgongo. 11. Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto. 12. Upungufu wa damu. 13. Maumivu ya kichwa. 14. Uzazi wa shida. 15. Kutopata ujauzito. 16. Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo. 17. Maumivu ya nyonga. 18. Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage). tiba unaweza kutumia tiba mbadala mbali mbali kuweza kutibu uvimbe hizi ni baadhi ambazo unaweza kujitibu ukiwa nyumbani. Tangawizi Mizizi ya tangawizi ni mizuri sana katika kupunguza maumivu na kuongeza msukumo wa damu. Andaa chai ya tangawizi (kumbuka ni tangawizi na maji tu, usiweke majani ya chai humo) na unywe kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa majuma kadhaa. Kwenye hiyo chai tumia asli badala ya sukari kwa matokeo mazuri zaidi. Chai ya tangawizi husaidia kuondoa uvimbe kwenye mirija ya uzazi na kwenye mji wa uzazi kwa ujumla Juisi ya limao Moja kati ya dawa nyingine za asili kwa kuondoa uvimbe kwenye kizazi ni juisi ya limau. Ongeza vijiko vijiko vya juisi (majimaji) ya limau na kijiko kidogo cha unga wa baking soda kwenye glasi ya maji ya uvuguvugu, koroga vizuri na unywe mara mbili kwa siku kwa majuma kadhaa. Kitunguu swaumu Kitunguu swaumu ni chanzo kizuri cha vitamini B6, vitamini C, na madini mengine mhimu ambayo husaidia kuweka sawa homoni za kike. Sifa yake ya kuondoa sumu mwilini husaidia kuondoa uvimbe kwenye kizazi. Kitunguu swaumu pia huzuia kujitokeza kwa uvimbe wa aina yoyote kwenye mji wa mimba (uterus). Tafuna punje 3 za kitunguu swaumu kutwa mara 3. Kunywa maji glasi moja kila ukimaliza kutafuna kitunguu swaumu kuondoa ukali na harufu mbaya mdomoni.

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU