Maumivu ya shingo na matibabu yake

Habari wapendwa, kipekee namshukuru Mungu kwa kunipa uzima na naamini mu wazima wa afya pia kwa uwezo wake. leo tena tunakutana kwenye makala zetu za kiafya na hapa leo tunazungumzia Maumivu ya shingo, njia za kujikinga zayo na pia matibabu yake. Maumivu ya shingo ni moja ya tatizo ambalo wanamichezo na watu wa kawaida limewahi kuwapata katika maisha yao ya kila siku, tatizo hilo huwa na maumivu ya wastani mpaka makali yasiyovumilika. Shingo kwa ujumla imeundwa na pingili za vifupa vidogo vilivyoanzia katika fuvu la kichwa. Katika ya vifupa hivyo huwa na santuri plastiki (cervical disc) ambazo hukaa kati ya pingiri moja na nyingine kazi yake ni kunyonya shinikizo la uzito na kuzuia msagiko. Vifupa, nyuzi ngumu za ligamenti na misuli ya shingo kazi yake ni kutoa msaada kwa kichwa na kuwezesha miendo mbalimbali ikiwamo pembeni na kujizungusha. Hivyo basi hitilafu, shambulizi au majeraha yoyote yanaweza kusababisha maumivu ya shingo. Chanzo kikubwa cha kujitokeza kwa tatizo hili ni kujeruhiwa kwa misuli ya shingo pale unapokuwa katika ulalo mbaya kama vile wakati wakulala usiku, wakati wa kucheza au mazoezi, kutumia kompyuta muda mrefu au kukaa katika viti vya katika gari, ofisini na nyumbani. Pia tatizo hili linaweza pia likawa ni shambulizi la mifupa pingili za shingo kutokana na kutumika na kulika kwa mifupa hiyo. Kuwahi kupata ajali, magonjwa ya shingo na matatizo ya mishipa ya fahamu. Hutokea mara chache kwa baadhi ya watu wenye dalili ya maumivu ya shingo likawa ni tatizo kubwa, mara nyingi huwa ni maumivu ya kawaida tu yanayoweza kuisha kwa siku chache. Kwa kawaida maumivu ya kawaida ya shingo huwa yanaweza kuchukua siku 2-5 yakawapotea yenyewe. Maumivu haya huwa ni kero na yanaweza kuwa makali kwa sababu shingo inapitisha mamia ya mishipa ya fahamu ndio maana huwapo na hisia kali za maumivu. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kuingilia mwenendo wako wakawaida wa kila siku. Yako mambo ya msingi yanayoweza kufanyika nyumbani ili kumsaidia mtu kutatua tatizo hilo au kulipunguza makali mpaka litakapoisha lenyewe. Njia rahisi katika siku za awali unaweza kuweka barafu na kuweka kwa dakika 10-15 katika eneo lenye kuuma, barafu iwekwe ndani ya katika mfuko wa kitambaa na unaweza kurudia kadiri ya uwepo wa maumivu. Baada ya hapo siku za mbeleni unaweza kutumia na kukanda kwa maji ya moto kwa kutumia kitambaa, au mfuko maalum wa maji moto au kuoga maji ya moto. Si mbaya kufanya usingaji (masaji) au kuchua kwa kutumia mafuta maalum au kutumia dawa za maumivu za ute mzito za kuchua. Mwisho unaweza kutumia dawa za kawaida za maumivu kwa ajili ya kukupa utulivu. Pata mapumziko ya kutosha na hakikisha unasitisha shughuli za kuchokoza maumivu haya. Epuka kulalia mto mpaka upone, epuka matumizi ya vitu kama kompyuta kwani vinachangia shingo kupinda wakati wakutumia na vile vile vitu vingine vitakavyosababisha kuinamisha shingo.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU