BAWASILI, DALILI ZAKE NA TIBA.

Bawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa kiingereza hujuliakana kama haemorrhoids au piles. Bawasiri inaweza kupelekea upungufu wa damu mwilini. Bawasiri inaweza kutibika ama kwa upasuaji ama kwa matumizi ya dawa mbadala kwa kipindi kirefu wiki hata 6 au hata zaidi kutegemea ilikuwa imejijenga kiasi gani. Bawasiri husababishwa na nini Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kupelekea wewe kupatwa na ugonjwa huu: 1. Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu 2. Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa 3. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile 4. Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu 5. Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana. 6. Kuharisha sana kwa muda mrefu 7. Kutumia vyoo vya kukaa 8. Kunyanyua vyuma vizito 9. Mfadhaiko/stress 10. Uzito na unene kupita kiasi nk Dalili za bawasiri 1. Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa 2. Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia 3. Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa 4. Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa 5. Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote Matibabu ya bawasiri: Kutegemea na umri wako na namna ugonjwa ulivyojijenga na kudumu, unaweza kuhitaji dawa moja au mbili au hata tatu kwa pamoja kati ya hizi zifuatazo. Kumbuka kumshirikisha daktari wako kabla ya kuamua kuzitumia hizi dawa. Dawa asili 6 zinazotibu bawasiri 1. Habbat-Sawdaa Chukua kijiko kikubwa kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa ukoroge ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara mbili kwa wiki mbili mpaka tatu hivi. 2. Habbat-Sawdaa na Asali Changanya gm 500 za unga wa Habbat-Sawdaa na nusu lita ya asali. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila baada ya masaa manne. Ukimaliza kulamba kunywa glasi moja ya maji ya kunywa ya joto la kawaida. 3. Aloe Vera Fresh Chukua kipande cha jani la mmea wa Aloe vera fresh (mshubiri) na kikate ukimenye kidogo ukitumia kidole kupata kama utomvu hivi au maji maji yake na upake sehemu ya utupu wako wa nyuma baada ya kuoga kutwa mara tatu. Jipake nyingi tu na uiache hivyo masaa kadhaa au mpaka utakpaoenda kuoga tena. Tengeneza pia juisi freshi ya mmea huu na uchanganye nusu glasi dawa hii na nusu glasi nyingine ya juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza nyumbani ili kupata glasi moja iliyojaa na unywe glasi 1 kutwa mara mbili kwa wiki 3 hadi 4. Juisi freshi ya aloe vera ni nzuri kwa kuongeza kinga ya mwili na kutoa taka zote za ndani ya mwili. 4. Juisi ya limau (lemonade) Chukua juisi ya limau na upake sehemu iliyoathirika. Juisi ya limau sifa yake kuu hapa ni kuondoa sumu na kuongeza kinga ya mwili kwakuwa ina vitamin C kwa wingi. Pia unywe glasi moja ya juisi hii kutwa mara kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja. Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi: *Chukua asali nusu Lita *Chukua limau kubwa 12, zikate katikati kila moja. Tumbukiza ndani ya sufuria na weka maji Lita 3, chemsha mpaka limau ziive (zisiive sana), ipua utowe zile nyama nyama za ndani za liamau moja baada ya nyingine, ganda la nje tupa na uchuje kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa lita 2 na nusu hivi. Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya ile asali nusu Lita na hiyo juisi ya limau Lita 2 na nusu, ongeza maji Safi ya kawaida Lita 2 ili kupata lemonade ya ujazo wa lita 5. Ihifadhi katika friji au kama huna friji andaa kiasi kidogo kidogo cha kutumia siku 3 kisha unaandaa nyingine. Kunywa robo Lita kutwa mara 2 kwa siku 10 hadi 11 hivi. Unaweza kuongeza vijiko vikubwa vitatu vya mdalasini ya Unga ndani ya hii juisi ya LEMONADE 5. Siki ya tufaa Chukua kipande cha pamba na ukichovyo ndani ya siki ya tufaa (apple cider vinegar) na ujipake kidogo kidogo eneo lenye uvimbe taratibu. Unaweza kusikia maumivu zaidi lakini jipe moyo taratibu yatapotea. Hakikisha unapata siki ya tufaa ile ya asili kabisa siyo ile iliyopita viwandani. Pia kama una bawasiri ya ndani yaani ile isiyojitokeza nje na ukaiona kwa macho moja kwa moja unashauriwa kuchanganya kijiko kidogo kimoja cha siki ya tufaa ndani ya glasi ya maji na unywe yote kutwa mara 2. Hii husaidia pia kupunguza maumivu. 6. Mafuta ya nyonyo Pakaa mafuta ya nyonyo mara mbili mpaka tatu kwa siku sehemu ya utupu wako wa nyuma kwa wiki tatu hadi nne hivi. Mambo mhimu ya kuzingatia ili upone bawasiri, bila kuzingatia haya itakuwa vigumu kupona kwako kupona ugonjwa huu: 1. Kula vyakula vingi vyenye faiba 2. Kunywa maji mengi kila siku ili kusafisha mwili na kuepuka kufunga choo 3. Kula sana mboga majani na matunda 4. Tumia mafuta ya mzeituni (olive oil) kwa wingi kwenye vyakula vyako 5. Epuka mapenzi kinyume na maumbile

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU