KIZAZI KUGEUKA

DALILI ZA TATIZO Kugeuka kwa kizazi ni tatizo ambalo mwanamke hawezi kuligundua mara moja hadi afanyiwe uchunguzi wa kina ndipo huthibitishwa. Pamoja na kulalamika kutoshika ujauzito kutokana na kugeuka kwa kizazi ambapo chanzo chake kinaweza kuwa maambukizi ya kizazi ‘PID’ au kushikamana kwa kizazi, uvimbe na mengineyo ambayo tayari tumeshaona. Mwanamke hulalamika pia maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara, maumivu ya kiuno, maumivu makali wakati wa hedhi na kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi. TATIZO LA KUTOKUSHIKA UJAUZITO Mwanamke ambaye amezaliwa hivyo kwamba kizazi chake kimegeuka huwa hakuna shida katika suala la kushika ujauzito, ila kwa yule ambaye kizazi kimegeuka kutokana na matatizo kama upasuaji, uvimbe, maambukizi, kasoro za tabaka la ndani la kizazi anaweza kupata tatizo hili kwa kiasi kikubwa kutokana hasa na mirija au njia za uzazi kuziba. TATIZO WAKATI WA UJAUZITO Wanawake wajawazito wenye tatizo hili la kugeuka kizazi hupatwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu wakati wa ujauzito, kadiri mimba inavyokua hubana kibofu cha mkojo na kusababisha maumivu wakati wa kukojoa au mkojo kutoka kwa shida katika kipindi hiki cha ujauzito. Kwa hiyo unashauriwa kama una tatizo hili uwahi haraka hospitali kwa uchunguzi wa kina na tiba. UCHUNGUZI Uchunguzi hufanyika katika Hospitali za Wilaya na Mikoa kwa madaktari wa akina mama, vipimo mbalimbali hufanyika kutegemea na jinsi tatizo litakavyogundulika. Vipimo vya ‘Ultrasound’, ‘Pelvic Examination’, ‘Speculum Examination’ ndivyo vinaweza kufanyika na vingine inategemea jinsi daktari atakavyoona inafaa.Mwanamke anaweza kwenda hospitali kutokana na sababu mbalimbali zinazohusiana na tatizo hili, mfano maumivu ya kiuno, maumivu chini ya tumbo, kuvurugika n.k kwa hedhi, kutoshika mimba.

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU