Mti wa mnyonyo ni tiba tosha kwa magonjwa

Mti wa mnyonyo ni tina ya magojwa mengi sana katika mwili wa binadamu Mti wa mnyonyo una faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Karibu kila kitu kinachopatikana kwenye mmea wa mnyonyo kina faida za kiafya kwa mwanadamu. Majani ya nyonyo ni tiba ya kifua kikuu na mizizi yake ni dawa ya mafindofindo, kuungua, macho yanjano, uvimbe, koo, kisonono na kaswende. Kikonyo chake ni dawa ya kwikwi. JINSI YA KUTUMIA MMEA WA MNYONYO KUJITIBU MAGONJWA NA MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA. Kwikwi : Jaza maji kwenye kikonyo, mpe mgonjwa anywe kila baada ya dakika 3 mpaka kwikwi iishe. Kuungua : Meza punje za mti wa nyonyo kwa maji kiasi cha glasi moja kwa siku kwa muda wa siku tano. Kutibu miguu inayo uma : Tumia majani kwa kufungia miguu inayouma. Maumivu Ya Mgongo : Majani yake ukiyapasha moto yafaa kukanda mgongo wenye maumivu. Kutibu Kaswende na Kisonono : Ponda mizizi ya mti wa mnyonyo, kisha chemsha na tumia kunywa glasi moja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba. Kuondoa Kondo La Nyuma : Mizizi ya mti wa mnyonyo ikitafunwa na mama mjamzito yafaa kwa kutoa mfuko wa uzazi ( kondo la nyuma ) kwa urahisi na usalama zaidi. Myonyo/Mbarika (Castor) ni mmea wa jamii ya Mbono Kaburi, kwa jina la kitaalamu Japtropha - Baadhi ya faida za mnyonyo na mazao yake. Mbali na kuweza kutumia mnyonyo kama uzio hai, njia hii inaweza kutumika kwa wale wasio na eneo kubwa la shamba ndiposa wakapata faida zake kama ifuatavyo: Majani ya mnyonyo yanaweza kutumika kama tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kukanda (massage) ili kuondoa maumivu na majani haya yakifungwa kwenye mguu unaouma huleta nafuu hasa kwa maumiviu yanayokuja baada ya kuteguka, pia hutumika kutibu uvimbe kwa wanyama. Mizizi ya mnyonyo huweza kutumiwa kama dawa ya mafundo fundo, uvimbe, kuungua, macho ya manjano, kuumwa koo na magonjwa ya kuambukiza ya kisonono na kaswende. Ukijaza maji baridi kwenye kikonyo cha mnyonyo na kumpa mtu mwenye kwikwi kila baada ya dakika mbili au tatu hivi, mara nyingi huondoa usumbufu unaoletwa na kwikwi. Mbegu/Punje/Tunda/Njugu za mnyonyo zikimezwa na maji bilauri moja kila siku kwa muda wa siku tano huweza kutibu maumivu yaliyosababishwa na kuungua Vile vile, mbegu hizi huweza kusagwa na kisha kuenguliwa mafuta kwa ajili ya matumizi mbali mbali Mbegu za mnyonyo kabla ya kukomaa Mafuta yatokanayo na mbegu za nyonyo mfano Ricinoleic Acid, Oleic Acid, Linoleic Acid nk hutumika kutibu ugonjwa wa wa jongo (rheumatism) unaowakumba watu wengi wanaoishi maeneo ya miinuko na baridi, pia hutibu ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama arthritis na gauti. Mafuta ya mnyonyo pia yanaweza kutumika kama njia ya kupanga uzazi kwani yana kiasi fulani cha sumu ya protini ijulikanayo kitaalamu kama ricin ambayo ikitumiwa kwa kiasi kidogo huharibu utungo, huweza pia kutumiwa kama mafuta ya kupaka ama losheni katika sehemu za siri ili kuua mbegu za uzazi za kiume wakati wa tendo la kujamiiana. . Mafuta ya Ricinoleic aci kutokana na mnyonyo vile vile yanaweza kutumika kurekebisha hedhi (mzunguko wa damu ya mwezi kwa wanawake) ikiwa mzunguko umechelewa ama kusimama katika umri usiotarajiwa. Huweza pia kupunguza maumivu makali yanayotokea wakati wa hedhi. kitaalamu kama Undecylenic Acid huweza kutumika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi na vidonda vinavyosababishwa na bakteria ama ukungu (fungus). Mbegu za mnyonyo baada ya kukomaa Akina mama wanao nyonyesha pia wanaweza kutumia mafuta baridi ya mnyonyo (kiasi kidogo ili kuepuka madhara ya mafuta hayo kwa mtoto, Nywele nzuri, safi, nadhifu na zisizokatika pia ngozi imara inapatikana kutokana na matumizi ya mafuta ya mnyonyo. Mafuta ya mnyonyo pia ni dawa nzuri ya kufungua tumbo la uyabisi (kuvimbiwa). Faida nyinginezo: Mnyonyo unaweza pia kuwafaa watu wanaoishi na VVU (Virusi Vya UKIMWI) kwani mafuta yake ni sumu ya kuua vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na ukungu (fungus). Njia : 1. Kupakaza: Chukua kipande cha nguo ama kitambaa, kisha kiloweke kwenye mafuta ya mnyonyo ndipo ufunge katika kiwiko ama eneo lenye maumivu ama kidonda. Vinginevyo, chukua kiasi cha mafuta na kupaka eneo linalohusika mfano, penye kidonda, kuugua ama pakaza kichwani au juu ya tumbo wakati wa maumivu ya hedhi nk. Unaweza kuacha kwa muda wa saa moja kabla ya kunawa ili uipe ngozi muda wa kunyonya kiasi cha mafuta. Unaweza kujifunga kitambaa hicho tumboni ama mgongoni kama kibwebwe na kuendelea na shughuli za kawaida. 2. Kunywa: Chemsha mbegu chache za mnyonyo pamoja na maji na maziwa kisha unywe kiasi kidogo kadiri ya nusu hadi bilauri moja ya ujazo wa mili lita mia mbili na arobaini. 3. Kusafisha utumbo: Kunywa mafuta ya mnyonyo vijiko viwili vikubwa vya chakula asubuhi, kisha pumzika kwa saa mbili ndipo unywe maji glasi mbili na endelea kunywa maji glasi moja kila baada ya saa moja. Kwa kujua namna ya kupanga uzazi wa mpango wa asili usiokuwa na madhara kabisa kwa kutumia mbegu za mnyonyo au mafta ya mnyonyo Wasiliana nasi tukusaidie Usitumie kiholela mbegu hizi omba ushauri kwa daktari anae jua faida na hasara za mmea huu

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU