Majani ya mpera hutibu bawasili,tatizo la hedhi na faida zingine 16

1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na kikohozi. 2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy). 3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi mwilini. 4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini. 5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume. 6. Pia inatumika kama scrub ya uso. Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni. 7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa ya kuponyesha tumbo la kuhara. 8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumia majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri kwa kupunguza maumivu na kukulinda na maambukizi ya bakteria. 9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa na mdudu na kupunguza maumivu. 10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina uwezo wa kutibu tezi dume. 11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi majani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibu chunusi. 12. Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguza uzito mwilini na kuzuia uharibifu sukari ndani ya mwilini. 13. Majani ya mpera yanajaza nywele na kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya nywele zako. 14. Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi, maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mpera na utaona maajabu ya majani haya. 15. Chukua majani ya mpera saga vizuri mpaka yawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kisha tumia kupaka usoni kama scrub inatibu ngozi inayoanza 16. mizizi ya mpera husaidia matatizo ya hedhi. chukua mizizi kadhaa chemsha kwa dakika kadhaa kunywa glasi moja mara mbili kwa siku kwa siku kadhaa pia majani yake yanasaidia kutibu bawasili.

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO ZA UZAZI

FAIDA ZA MAJANI YA KIVUMBASI

BANKING SODA NA U.T.I SUGU