ZIJUE FAIDA ZA LIMAO MWILINI
Hizi ni faida saba za maji la limau kwa mwili wako. 1. Husaidia kuongeza maji mwilini Kulingana na wataalamu wa lishe mtu mwenye afya bora anahitaji kunywa maji kati ya lita 2 na 5 kila siku. Maji haya ni pamoja na maji kutoka kwenye vyakula na vinywaji. Maji ndicho kinywaji bora zaidi cha kuhakikisha mwili una maji ya kutosha, lakini badhi ya watu hawapendi maji kawaida. Kuongeza limau husaidia katika kuyafanya maji kuonya vizuri, na huweza kukupa hamu ya kunywa maji mengi zaidi. 2. Ni nzuri kwa vitamini C Ingawa sio moja ya matunda yenye virutubisho vingi vya vitamini C, limao ni bora kwa kuwa kemikali mimea ambayo hupatikana katika tunda hilo husaidia kutibu mafua na mfumo wa upumuaji. Maji ya limao yanatajwa kuwa na takriban miligramu 18.6 za vitamini C. Na vipimo kamili vya kila siku vinavyopendekezwa kwa watu wazima ni kati ya miligramu 65 na 90. 3. Husaidia katika kupunguza uzito wa mwili Utafiti umeonyesha kuwa virutubisho vilivyo katika limau kwa kiasi