Posts

Showing posts from October, 2019

BAWASILI, DALILI ZAKE NA TIBA.

Bawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa kiingereza hujuliakana kama haemorrhoids au piles. Bawasiri inaweza kupelekea upungufu wa damu mwilini. Bawasiri inaweza kutibika ama kwa upasuaji ama kwa matumizi ya dawa mbadala kwa kipindi kirefu wiki hata 6 au hata zaidi kutegemea ilikuwa imejijenga kiasi gani. Bawasiri husababishwa na nini Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kupelekea wewe kupatwa na ugonjwa huu: 1. Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu 2. Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa 3. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile 4. Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu 5. Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa n

Dawa za asli za kutibu chunusi

DAWA ZA ASILI 20 ZINAZOTIBU CHUNUSI Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni. Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria. Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris. Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17. Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents). DAWA ZA ASILI 20 ZINAZOTIBU CHUNUSI 1. Barafu Dawa ya kwanza katika orodha hii ni barafu. Barafu inaweza kuzipunguza chunusi zionekane ni ndogo na kupunguza madhara yatokanayo na chunusi. Namna ya kutumia barafu kutibu chunusi ni rahisi na haraka zaidi. Chukua kipande cha barafu na ukipitishe sehemu zilipo chunusi mara kadhaa kwa dakika 3 hadi 5 hivi. Kumbuka kusafisha vizuri uso wak