KIZAZI KUGEUKA
DALILI ZA TATIZO Kugeuka kwa kizazi ni tatizo ambalo mwanamke hawezi kuligundua mara moja hadi afanyiwe uchunguzi wa kina ndipo huthibitishwa. Pamoja na kulalamika kutoshika ujauzito kutokana na kugeuka kwa kizazi ambapo chanzo chake kinaweza kuwa maambukizi ya kizazi ‘PID’ au kushikamana kwa kizazi, uvimbe na mengineyo ambayo tayari tumeshaona. Mwanamke hulalamika pia maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara, maumivu ya kiuno, maumivu makali wakati wa hedhi na kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi. TATIZO LA KUTOKUSHIKA UJAUZITO Mwanamke ambaye amezaliwa hivyo kwamba kizazi chake kimegeuka huwa hakuna shida katika suala la kushika ujauzito, ila kwa yule ambaye kizazi kimegeuka kutokana na matatizo kama upasuaji, uvimbe, maambukizi, kasoro za tabaka la ndani la kizazi anaweza kupata tatizo hili kwa kiasi kikubwa kutokana hasa na mirija au njia za uzazi kuziba. TATIZO WAKATI WA UJAUZITO Wanawake wajawazito wenye tatizo hili la kugeuka kizazi hupatwa na