Posts

Showing posts from November, 2019

dawa na namna nzuri ya kufuga kuku

Kuku wa kienyeji nao wanahitaji kupata chanjo ya magonjwa na kwa utaratibu unaofaa. Chanjo kwa kuku wa asili Ugonjwa Jinsi ya kuudhibiti Mdondo/kideri (Newcastle disease) Kama tete lilichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki tatu za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hawa dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18. Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku ya 3 mara baada ya kuanguliwa, rudia wafikishapo wiki 3, kisha uchanje kila baada ya miezi mitatu (3). Ndui ya kuku Vifaranga wapewe chanjo ya kuzuia ndui wafikishapo umri wa mwezi mmoja. Ukosefu wa vitamini A Watafutie kuku majani mabichi au hata machicha mara kwa mara. Kama hakuna majani wape vitamin ya kuku kutoka dukani kama ziada. Ugonjwa wa kuharisha damu (coccidiosis) Safisha banda kila siku na hakikisha hakuna unyevu sakafuni. Wape vifaranga dawa ya kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu kwa muda wa siku tatu mfululizo mar